Signed in as:
filler@godaddy.com
The New York Tanzanian Community is a 501(c)(3) non-profit organization registered in the great state of New York.
Hayawi hayawi sasa yamekuwa! Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania NY, NJ, CT na PA (NYTC) unawakaribisha wanajumuiya wote kwenye BBQ kali ya mwaka! Watoto, ndugu, jamaa na marafiki pia wanakaribishwa.
Kutakuwa na Muziki kutoka kwa DJ wakali DJ Mao na DJ Richard, Michezo ya watoto, Nyama Choma, Vinywaji, after BBQ party, na kadhalika. Pia tutakuwa na fursa ya kuwasikiliza Viongozi wetu kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Jumuiya yetu, hususani suala la mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba na usajili mpya wa wanachama.
Mgeni rasmi siku hiyo anatarajiwa kuwa Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Mheshimiwa Balozi Hussein Kattanga.
Kama ilivyo ada, ukiwa kama mwanajumuiya tunaomba Support yako ya mchango ili kufanikisha shughuli yetu. Wachangiaji wote watapewa Wristbands maalum watakazozivaa mkononi wakati wote ili kupata huduma na kutambua juhudi zao za kufanikisha shughuli yetu, ambayo pia ina lengo la kutunisha mfuko wa Jumuiya. Suggested donation ni $100 kwa familia.
Tafadhali tuma mchango wako kwa Kinyasi Monyi kupitia:
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na:
Soma Flyer iliyoambatana na hili tangazo au BOFYA HAPA kwa Taarifa zaidi kuhusu Siku, Muda, na Mahali itakapofanyika BBQ yetu.
Karibuni nyote!
IMETOLEWA NA;
UONGOZI-NYTC
JULY 10, 2024
Ndugu Wanajumuiya,
Uongozi wa Jumuiya unapenda kuwakaribisha kwenye mkutano wa Wanajumuiya na Viongozi wake utakaofanyika siku ya Jumapili, June 9, 2024 kuanzia saa 1 kamili Usiku (7:00pm) hadi saa 3 kamili usiku (9:00pm). kwa njia ya Zoom.
Mkutano wetu utakuwa na agenda zifuatazo:
1. Utambulisho mwingine wa Viongozi wa Jumuiya na wajumbe wa Kamati za Jumuiya.
2. Kutoa Mapendekezo na kupokea Maoni kuhusu Mabadiliko ya vifungu vya Katiba kuhusu masharti ya Uanachama na benefits za uanachama, kabla ya kuwasilishwa kwa Bodi kwa ajili ya utekelezaji.
3. Kuanza kwa mchakato wa Usajili wa wanachama wapya na wa zamani kupitia database kwenye website yetu.
4. Kuanzishwa kwa Program za Ushirikiano (Partnerships) zenye manufaa (benefits) kwa wanachama walialipa ada za uanachama.
5. Mkakati wa kuhimiza wanachama kujiunga na program za kusaidia kipindi cha misiba, na ushirikishwaji wa viongozi wa jumuiya pale misiba inapotokea.
6. Kalenda ya Sherehe za Jumuiya kwa mwaka mzima, pamoja na kuanzishwa kwa “Quarterly Zoom Town Halls.”
7. Mengineyo.
Unaweza kujiunga Mkutanoni kupitia Zoom kwa kubobyeza link hii: https://tinyurl.com/NYTC-Zoom-meeting
Meeting ID: 848 2697 9824
Passcode: Wasiliana na Uongozi kupitia group la Jumuiya Whatsapp.
Ahsanteni,
Uongozi - NYTC
06/052024
Ndugu WanaJumuiya,
Uongozi unapenda kuwashirikisha kwenye Muhtasari wa yaliyojiri kwenye Kikao chake na Kamati ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kutathimini Ufanisi wa Utendaji kazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliofanyika Alhamis Juni 8, 2023 kwenye Ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Uwakilishi wa Kudumu Umoja wa Mafaifa.
Muhtasari huu wenye kurasa tano (5) unaweza kusomwa moja kwa moja kwenye website yetu au kwa kupakua (download) na kuusoma offline kwa kubonyeza PAKUA MUHTASARI hapo chini.
Ahsanteni,
Uongozi NYTC
Wajumbe wa Kamati ya kufanya tathmini ufanisi wa Utendaji Kazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, iliyoteuliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, inategemea kuwa na mkutano wa kukusanya maoni na Viongozi wa jumiya za Watanzania (Diaspora) siku ya Alhamisi, Juni 8, 2023, ndani ya ukumbi mikutano za ofisi za Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania, Umoja wa Mataifa.
Ajenda kuu za mkutano zitakuwa kama zifuatazo:
1. Ushirikiano wa Diaspora na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
2. Mchango wa Dispora katika ujenzi wa diplomasia ya kiuchumi
Wanajumuiya wanahimizwa kuwasilisha maoni yao kupitia viongozi wa jumuiya kupitia group la WhatsApp la Jumuiya, kwa email ya jumuiya info@nytanzaniancommunity.org au kupitia fomu (Bonyeza kitufe cha Wasilisha Maoni yako Hapa ) iliyoambatanishwa na Tangazo hili.
Maoni yatakusanywa kuanzia leo Jumatatu, Juni 5, hadi siku ya Jumatano Juni 7, 2023.
Ahsanteni,
Imetolewa na Ungozi NYTC
Updates Juni 8, 2023: Muda wa kukusanya Maoni Umeshapita. Fomu ya kuwasililsha maoni imeondolewa.
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya WaTanzania New York City na Viunga vyake, Bw. Nathan Chiume, kwa mashauriano na Bodi ya Wadhamini (Board of Trustees), na Kwa matakwa ya Katiba ya Jumuiya Sehemu ya 3.6 inayompa mamlaka ya kuziba nafasi za wazi kwenye Uongozi wa Kamati Tendaji (Executive Committee), ameteua Viongozi wapya wafuatao:
1. Dk. Mwemezi Basil Deusdedit kuwa Katibu Mtendaji wa Jumuiya
2. Dk. Nyemo Mbennah kuwa Naibu Mweka Hazina wa Jumuiya
Aidha, kulingana na Katiba ya Jumuiya sehemu ya 3.10 (m,n,o) inayompa mamlaka Mwenyekiti wa Jumuiya kuteua wajumbe au Kamati Maalum ya kusaidiana na Kamati Tendaji, amemteua
1. Mhandisi Kinyasi Monyi kuwa Mkuu wa Masuala ya Teknolojia ya Jumuiya.
Uteuzi huu unaanza rasmi Mei 30, 2023.
Dr. Mwemezi Basil Deusdedit - Secretary
Dr. Nyemo Mbennah - Deputy Treasurer
Eng. Kinyasi Monyi - Chief Technology Officer
Mr. Nathan Chiume - Chairperson
Mr. Gaston Mkapa - Deputy Chairperson
Ms. Victoria Mwanyonga - Deputy Secretary
Mr. Sam Mfalila - Treasurer
**The board of trustees has suspended the requirements for active membership (Yearly fees) in this election cycle**
We are dedicated to improving the lives of those in our community. Your contribution today helps us make a difference.
Copyright © 2024 New York Tanzanian Community - All Rights Reserved.